Total Pageviews

Wednesday, 6 September 2017

Timo na Ngori Za Mtaa- SHENG series imechorwa na Mwas Mahugu




 Timo na Ngori Za Mtaa- Sheng series imechorwa na Mwas Mahugu




Kayole - town ilikua imetulia sana especially ka ulikua umetoka the other side of the town,kaa ungetaka ku-rejuvinate mind,kupata ile inner calm yak u-enjoy nature,basi hii ingekua your perfect escape,ni vile tuu sometimes kulikua frequent gun exchange ya mabang'a na madingo,hizi streets exchange zilikua fun kwa watoto wa primo,since chuo zikifungungwa walikua na version tofauti ya “Godi sinya”walikua wana make gun za wire,na rubber bands,na whole day ilikua ni cat and mouse kwa alleys za k-town,naughty boys sometimes wange shoot buttocks za wamatha,games zilikua mob taya,bano,cattie,
Watoi machokosh ndio tuu walikua washajua hustle before,wali spend the whole day waki collect carton peppers,plastic,machupa,na ma-srcap metal..sometimes watoi wa estate wange simamisha game zao za guns za wire,na ku scream in unison “”chokora mapipa chokora mapipa”na immediately tu-wars tulikua tunaanza,wakishoot.but ma chokosh walikua wana give up juu always walikua-anga super dupa high na chupa ya glue,lower lip ilikua ina suspend na kushikilia hii,hata mbio gani! hainge fall.
Street za kuingia k-town zilikua za nguvu, artificial flowers za miscellaneous colors,zimepangwa all over na design ya abstract na ma  provided na officio  department ya  garbage collection ,hawa wasee walikua wame advice raiya kumwaga soil kwa hizi roadii za mtaa ili kufunika lami,solar ikiwa hot lami ilikua inachoma watoi miguu waki-ride ma-tyres,hii issue ilikua inaleta ma-parent  juu:reason being after mtoi ku-burn na lami alikua anarudi home na statement kaa hizi zilikua za kawaida””aaahhh woishe Mama nivae viatu za shule leo pekee?”nimechomeka sana.

‘’’NGRRRRi krriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiing, bell ilimalaizia
Watoi wali-ignore bell na kundelea kucheza ball ya ma-paper,ilikua ni break time ya afternoon,kitu 4pm,middle classes zilikua zisha go home,na maboi walikua wana jibamba,Moodee yani alitokea from no where!
“Hey boys it is time to go home,play time is over go home.teacher alli-annouce loudly

Timo ana grab ball speed speedie na bila ku-respond anatoka teke teke akifuatwa na ma-boys wengine.
Teacher naye aka- head back kwa classes,kayole town primary school,imejengwa poa,concrete walls na roofing ya grey asbestos, ilikua chuo ya nguvu.
After dakika kadhaa Timo wali slow down after kupenya kwa mtaa,walikua wana hema sana juu bag heavy  ya books nyuma ya mgongo .
Timo:Manze jo mo-dee amekatisia game mbaya
Beste: Timo manze nilikupiga chobo!! Ha ha ha
Timo :na na  nani? Nani? Sura ka chobo!! Ha ha
Beste: umenza mchongoano?
Beste 2:kaende kaende mimi ndio refa,boi mwingine wa tatu alichangia
Soon walisimama na ku form a circle na mchongoano ikaanza.
Sky ilikua radiant ,miale the solar zilikua zinaptia hii mtaa golden rusty color ya nguvu,ka sun sun set kalikua ka na take cover ,wasee wa kupika mandazi , walikua wanarudi bizness round two!baada ya kuamkia biashara ngware,fishmongers,mutura ,supu,nyam chom round ya kwanza, waki expect booming business ,wasee wakitoka job,na watoi wakirudi home kutoka chuo,jamaa wa ice cream alikua busy whole day,na solar ilikua ina mshow time yake ya kufunga biz ilikua isha fika,alikua ana chezea ma injury time ,idhaa ilikua ni ma five.

Msee wa kuuza miwa alipita, na Baba Timo aka mwita,
“tukatie na utu chongee ya 20 bob”na ugawanyishe mara mbili,baba Timo ali show Msee wa miwa.
Baba Timo.: rafiki mambo yamekua magumu, (alisema huku aki clear throat)
Jirani:Si kwako tuu,ni kila pahali,ni kawaida ya maisha
Baba Timo:hata siamini ni huyu motto wangu <
Jirani: amefanya nini tena?
Baba Timo :ana bidiiii sana shuleni,tabia nzuri naomba mola nihakikishe amefika chuo kikuu rafiki!
Trader wa kuuza miwa ana maliza kuchonga miwa na ana pass kwa Baba Timo na rafiki yake,but wote wanapatwa na surprise ,
“Hata mimi na taka miwa baba,Timo anadai huku amebeba bag na paper bag kwa mkono.
Baba Timo:haya mchongee ya 10 bob anamwambia msee wa miwa,hukua akimgeukia mtoi wake Timo
“umetoka wapi?usiniambie tena pia umeokaota okota hivyo vyuma?aaaha?
Timo:mbuyu unajua tumesota,mee nita uuza hizi tupate za chakula ,na wewe ulipe karo
Baba Timo(defeated)basi ingia ndani wenzako wako ndani
Aha ha ha jirani anacheka kidogo “watoto wa siku hizi!
Baba Timo :wamuona weekend zote hushinda akiokota hivyo vyuma juu hakuna shule
Jirani:atakua mtu wa heshima  kwa jamii,sio kama hawa!una waona,:
jirani ana-point jamaa wawili wanapita street wakistagger, “wamesomeshwa halafu baada ya hiyo bidii yote na pesa matokeo ndiyo haya”!
Baba Timo:muone hata hana haya ana kojoa hadharani!
Drunkard wa pili pia ana move kwa wall na pia kunyoraa,without giving a damn.
Crow ikoo juu ya green street light ime spoil,malibou stock ziko juu ya mitii mbili za acacia zilio kwa hii street,na pia kuna moja ina hop hapa na pale,ina limp.next na  non approved refuse pit next kwa stage,
ma bachelor na wasee wakurauka ngware ndio chanzo ya pile  ya garbage  kwa hii street , hao huanza one paper bag ,siku ya pili two,na soon ,kila mtu wakurauka job early ana follow na uchafu yake na soon after,uchafu kupile up.

Timo anascavange for scrap metals na ma-plastic,kwa hii dump pit,anavunja upande wa kushoto na achecki original street Boy aki approach,kwa kawaida machokosh wa mtaa huita boy ka Timo mbagishon ,slogan ya chokosh msafi
Street boy 1,tulikwambia hii si job ya wasee wako chuooo,weee ruudii shuuule!
Street boy2:first leta hii    zii .
Street boy anamnyang’anya Timo collection yake,huku Timo aki-refuse
Aaaaaaaaachilia chokosh wapilia anadai huku aki mshika kidevu,Timo ana-fall,na machokosh wanatoka teke teke.


After sometimes, bongau ama kama hushiki malibou stock ina shonde kwa face ya Timo ,na hako ka baridi kana mrudisha kwa consciousness yake,ana walk home mdogo mdogo,huku aki breed kwa lips kiasi,
Bell ya msee wakuza maziwa ya brookside,inamrudisha kwa flash back,hio incident ili-happen akiwa eleven years,3 years ago,na sasa alikua fourteen years na candindate,Timo alikua ame lean kwa wall behind class eight classes,
On the front side,ni celebration,pupils washikilia exams pads na geometicals sets,hewa imejaa happy voices na murmurs,jumping up and down,hugs na kisses,wote wana celebrate Kumaaliza Kenya certificate of primary education(KCPE)exams
Timo ana-wajoin lakini  amevaa sura ya kazi
Pupil:checkini huyu msee(all attentions kwa Timo as murmurs zina die)
Pupil 2:sura ya kazi ya nini?shida ya nini?
Pupil mwingine anatokelezea na teje boom box ya nguvu huku ame  beba  kwa shoulder,attention ina leave Timo
Boi:Ha ha ha Njoro umechukua teje ya home kwenu?kichwa yako mbaya!
Njoro: hei hei msee wangu kua mpole nina ma- mix mwenda after all exams zimekatika
Ana switch on teje “ a big tuuuunnnee,… a horn blast, DJ bunduki on the mix!”the rough and toughest this is followed by a raggaa riddim,and everyone is dancing.inabidi madame wainue skirt kidogo hadi kwa knees ndio waweze kuziondoka,na kila boi alishikilia manzi kutoka nyuma.


The same Dj mixx inaendelea kuchuna kwa Matatu,raia ni wengine ,horns za magari kila pahali,makarao,ma-hawker, mabroker,ma-hustla ,ma-sonko,Timo anauza njugu.
“nani mwingine?nani mwingine?
Mara msee anamvuta kutoka nyuma!raia ni ku-stare tuu kawaida ya Kayole
Stranger: we fala nani alikua mbia unaweza uzia njugu hapa?ana uliza kwa ukali
Timo:ati nini kaa huna doe ishia!Timo anajibu kwa ukali
Stranger  ana –move next na Timo kumushika mashati na kumkaribia kwa face,pia boi mwingine ana join na soon Timo ako surrounded na rende ,msee mmoja anachukua njugu tano,
Na ku-point Timo “wee fala na uchunge line zetu
Timo:fala ni wewe na ulete doe ya njuguu,tusi zoeane sitaki ngori
Mara ngumi heavy ina mpata Timo,ikifuatiliwa na ingine kwa kahasho,Njugu zina fly kwa hewa na Timo hajui kaa anaona njugu ama ma stars! noomaa.jo




Baba Timo ameshikilia gazeti,aki chill food,na kwa korner ingine ya room Mama Timo analeta plate ya tilapia fish na ugali,kama kawaida inawekelewa kwa table ,sister na bro wa Timo  wana-salivate waki wait mchezo wa meno.
Baba Timo.kila siku samaki ugali,kila siku samaki ugali!kwani majirani wamekufunza nini?
Mama Timo:kwanza samaki ina demand sana tafuta pesa ufungue kibanda,wacha maneno ya kutafuta kazi..hujui hakuna kazi baba
Baba Timo:pesa ziko wapi?mama watoto,Timo huyo ana faa a join form one
Mama Timo:lakini baba watoto si wale watu wa NGO wanalipa karo
Baba Timo,wanalipa 80% na sisi 20 % na tununue uniform!
Mama Timo:usijali mungu atatuonekania
Family ya baba Timo ilikua na watoto watatu,vijana wawili na msichana mdogo,Timo alikua ameachwa na miaka tano na Toni ,Timo alikua 15 years old,na ready kujoin form one,wazazi wake walikua proud na biidii yake especially after Kcpe,Timo alikua a young hawker in Nairobi town,hii bidii ndio ili-attract mama Timo kwa Baba Timo,but nowadays mama Timo alikua ashaboeka na Bwana yakee,juu alikua asha kua m-lazy,alichunjwa job,5 years ago na akakua alcoholic,na ku-loose any drive ya creativity na pia morale ya kusaka job.Baba Timo alikua na ana leave in denial na pipe dreams,za kurudi job kwa Samken logistics kama machine operator,Mama Timo alikua ashachoka na version yake ya reason ya kuchunjwa job,Baba Timo alikua ana dai eti alikologewa na kutupiwa majuju,na workmates wake,but the heart of the matter kampuni zilikua zina streamline workers,juu ya hard financial times.
Mama Timo ndiye alikua bread winner pekee ,alikua ana uuza second hands clothes gikomba,but off late alikua proud of his son Timo juu ya back up,from his hawking business.how ali-wish twin yake angekua.alikua ana leave na regrets za kupatiana one of the boy to adoption.but hakua na choice,walikua so broke na jobless fifteen years ago,na walikua wanaishi Koch shanties,nyumba za matope ,na mabati za drum,although hawakua wame piga progress sana but now ,walikua wanaishi kwa plot nyumba ya Mawe na toilet walikua wanashare na wasee wengine saba,kwa bafu ama toilets asubuhi ndio the only way ungejua majirani,juu sometimes walikua wana patana hapo,na ilibidii ku-que In turns,so they all knew Yule msee akiingia toilet mbele yako,ni mambo badd ,,pia hii area ya toilet na bafu ndio ilikua place ya kufulia na pia,platform ya mpango wa kando,amenities zote communial ,zilikua hapa pia sink,zote zilikua mwisho ya plot.
Kulikua na siri za kila plot,nani hu hanya nani?nana hupiga wife usiku,mlevi na pia nani ameokoka,most Fridays kulikua na Jumuiya wa wakristo,na wasee wa church wangekuja kwa mama Timo ,kwa maombi,times kama hizi .Baba Timo alikua missing na ungempata Kahuruko base,akinywa barley na wazee wenzake,wote walikua na same stories vile walikua na pesa kitambo,before shetani atokee kwa life zao.
Nyumba ya family hii,ilikua one room,na kulikwa na curtain imegawanyisha keja mara mbili,Timo alikua akilala kwa sofa na wataoi wengine waliktandikiwa chini,for the last 3 years sex life yao ilikua affected sana since,mama Timo felt,Timo was a young adolescent man,and so alikua amechill,but the real truth was since Baba Tonni aingilie pombe,alikua asha kua one minute man na time mob,Mama Timo alichwa hanging’but alikua asha jipanga na bwana wa jirani,so waliishi hivyo.naye Baba Timo alikua ana pata service kutoka kwa Bar maid wa kahuruko,according to rumors kutoka kwa wamama mabeste wa mama Timo,zilisema pia Baba Timo ndiye alikua analipia Bar maid waithera nyumba,but since Baba Timo amu slap ones alipoenda kumake enquiries ,3 years ago,She shut up,na akatafuta mpango wa kando.although alikua ana feel guilty kila siku,na alikua ana ogopa watoto wajue..
Mara mingi scandles za mapenzi zili-kua zina fichuliwa na watoto wakichongoana innocently
“Wee nyamaza na mama yako hukuja hukuja kudowea food kwetu”wakati mama ametoka once a neighbor son told Timo 4 years ago,but luckily hakukua na watu kwa plot.
Timo ali amka huku amechangayikiwa,aliokota njugu zake,akirudisha kwa basin but mob zilikua zishakanyagwan na raia,mara askari wa Kanjo akatokea,na ku-knock Timo na boots zake
Askari:wewe nyanga’u unafanya sarakasi gani hapa?
“Nimepigwa na wakora ‘Timo alijitetea
Askari:wakora wagani ?amka kwenda nyumbani,ama nikutupe kwa lorry,wewe ni motto mdogo
The council askari alim-slap kwa mgongo,Na Timo alisahau njugu zake na kupotea mbio,alikua ashasikia story za kufungiwa juu ya hawking,Timo alishika njia ya river roadi ndio ateremke Otc achukua mat,after dakika kadhaa,one hundred metre ndio afike kwa stage yake,alishangaa watu walikua wakiscream all over ,loud bangs za milango za business zikifungwa,carn horns, mara smoke ikajaa kwa hewa,haikuchukua time mob before Timo ajue ni Tear gas ,alikimbia Nduki,na kuchukua alley tofauti,hakua ana ona vizuri kila mtu alikua kiguu niokoe, mara kwa mara  alingona na watu,but ilikua ni Kiguu ni ponye.
Hali ya taharuki ilikua ishajitangaza,watu wakikimbia kila place,Timo ali slow down!
Kando ya road mwanaume alikua amelala chini,in seconds kila mtu alikua akisimama kidogo na kundelea kukimbia,damu ilikua itiririka kutoka kwa mguu,Timo alizubaa kiasi but network ku-rudi na reality,ali run na kundandia matatu,alipata seat next na mzee flani.na kutry ku-relax.
Huyo mwanaume ni mwizi..mzee aliuliza
“Sijui,Timo alijibu
“amekufa ? sauti ingine iliuliza
“Nadhani “Timo alijibu huku akipumua
“wacha wakufe hawa wezi ndio wana tuhangaisha usiku”sauti ya manzi ilichangia kutoka back seat.
“ameiba nini?mama alikua kiti mbele aliuliza
“eti mkate!sauti ya mzee nyuma yetu
“ wacheni fitina mimi nime ona na macho yangu ,alikua hawker amenuizia kitambaa,dakika chache kabla city council askari wampige! Huyo sio mwizi,mama alikua na machungu na huruma aliongea.
Conversation zikaanza,na soon kila msee akaanza kupeana version yake,hata walevi walichangia, after kuchoka,kila mtu akanyamaza,after time music sytem ikaashwa
Feeling na atmosphere ina change,viti niza velvet ,graffiti na portraits za mean face black American stars zina ni stare nika tuna-beef bado!

…Noma noma..noma riddim flani ya ragga ina –blast kutoka kwa ma –woofer,macho zote za passenger ziko glued kwa plasma screen,scenario ni palms trees,aqua blues sky kwa background,Jamaican Artistes ndio main attraction,but kwa side show,kuna scantly dressed ladies na ma-bikini.
, unexpected abrupt breaks ,hu-ku-force ukae sober,hakuna cha day dreaming kwa Nganya,nikushikilia ile kiti iko mbele na mikono miliwi,otherwise kichwa yako itagonga ceiling ya mat,na impact ya kurudi kwa kiti pia ,inaumiza especially ka mathutha zako hazina enough shocks absorbers,
madere hawana huruma,na pia sikupenda kwao idhaa haiwarusu.ni paper chase,na kwa roads za Nairobi wana rule,ku-break rules nikawaida ka macho ku-blink,ku-break rules ndio law,Matatu ina stop abruptly, suddenly policeman amevaa sura ya kazi anaingia na ku-uangalia,kila mtu amenyamaza,ngoma ilizimwa kitambo.

We conductor wapi kiti yako?
Koni-kodi anamvunjia na design flani,karao anashuka,na conductor anamfuata nyuma,after dakika mbili,kuna loud banging ,simultaneously mat ina-move,


Vj a.k.aDj kalonje ndio ako on the wheels of steel ,ngoma inarudi ka kawaida.entertainment full blast,woofer zinachuna karibu zi-blow heart ya msee injebaada ya muda .

Timo alishuka matatu, na ku-ingia mtaa wa K-town,watu walikua wengi na pia biashara za jioni zilikua mob,music hawkers walikua busy na Tv zao kwa street wakuiza cds na movies na Dvd,wamatha walikua wakikatia watu mboga kwa kiosk,harufu ya fried fish na burnt animal fat kutoka kwa nyama choma joint ilikua all over,
k-town usiku giza ilikua totoro,murmurs ndio zilikua kibao,once in a while unge-nywesiwa na bike,ya ma-milk vendors waki deliver maziwa ama mikate,butchery zilikua na customers na pia ma-shop,but watu walikua busy ilikua wasee wa kuuza mutura ,maini, na soup,so among the murmurs sounds ilkua ina sikika sana ni ya msee wa soup aki-i-beat kwa kibuyu,clad na white dust cost ,
Once in a while ungesikia ma-nduru uki –walk kwa hizi street,most def ilikua ni either ka -newborn baby kamewasili..Story za hosi zilikua ni fyam.hakukua na dawa,juu zote zilikua zishauzwa kwa ma-phamancy za mtaa,pia story ya the famous pastor Deya ilikua inachangia sana..Ku-delivier kwa hosi chances za mtoi wako ange disappear miraculously zilikua high sana.
Nduru ya pili :ungesikia kwa same street ni ya msee akipigwa touch!yani ngeta kwa ufupi,ka-evening rush ka mabuda kupeleka ka nyama quarter home baada ya kuangusha tu-kilo kadhaa na mabuda wenzake..ilikua ni celebration kwa petty thieves wa K-town .sana sana walikua ni walevi na sometimes sober,vitu zilikua zina move fast. kwa hii street unge-checki nyuma ama sides just ku-make sure your ass is not the next one on-line,hii ilikua street reflex, hata ka ni gun shot zilikua kwa hewa..kila kitu ilikua ni kawaida no big deal,although resident walikua wanatoa tax kwa self appointed community policing,kulikua thin line between ma-dingo na security.
Nduru ya tatu: ilikua ya any body .admist hizi fracas Makarao walikua wana- supply mwangaza for a while.but resident walikua wana pay heavily for the light.mataa ya ndai ilikua always full light,ilikua ina-stand far,ma boi wa kiganjo..Maboi wa murungaru..Kwekwe.. Spider.. ma-beast..mambang’a e.t.c names zilikua endless,walikua wana ndondoka na ku-spread huku waki –ji-mix na raia.so nduru yetu ya tatu ilikua ni ya kibaree ama kama huelewi na maanisha kofi.either ya kijana amepatikana na twenty bob kwa mfuke pekee yake,ama ya mother alikua amekuja kutetea motto wake
Mama “mnashikia Kijana wangu nini, nime memtuma kwa duka tuu saa hii!
Mbang’a “ twaaafff! Ki-baree ya nguvu!) mama tunamjua mtoto wako,ni jambasi tumemtafuta sana”
Scenario kaa hii the only option ilikua nu ku-rush kwa mattress account ama akope-mama mboga Wamercy.soe moja ili mtoi wake aachiliwe.every resident alikua vulnerable ku-transformiwa pesa point kwa hako kagiza.pingu ndio ilikua A.T.M card.
Nduru ya inne: ilikua lovely.all roads after hizo drama zote zilikua zina lead to of course kejani. Plot zilikua zimeshikana bampa kwa bampa some za ngoro yani high rise.every plot ilikua na approximate watu fifteen, so ka ni ngoro una multiply,although Country yote ilikua na receive heavy rain downpour,still power rationing zilikua ni zaa kawaida ka oxygen,rationing ingeisha aje,na ma-Minister ama ma- Mps, ndio walikua wanauzia Kayole Gen power. Generators za kutumia diesel ndio zilikua zina churn electricity,but according to officios report,a foreign company ndio ilikua imepewa tender..ili ku-ease rationing,for all those years hata after LA-Nina Na EL nino ku-come watu hawa-kusikia rationing zimeisha.so back kwa nduru yetu ya nne,
ilikua nyuma ya ma-candle lit dinners,after-ku- watch news..ya the same same boring Leaders with same same old script. anglo leasing, golden berg.maize scam triniton deals a scandals ,Citizen protest,l ast but not least KCC ikimwaga Thousands litres of milk,ka-ghetto queen ange serve buda,na ku-take position watching South american soaps ama Nigeria movies,after hapo ni slumber land.soo kwa –meda sometimes ilikua inanza early.ma-lovi davy.

Scenario ilikua the same Koinange street,but on that side ilikua ni between city officios, perverts and thieves in such of pleasures versus thigh-land squad caught up kwa paper chase ili walipe bills,raising children ama colleges fees.na usisahau Sunday morning church service hii squad ndio walikua may be biggest contributors, to the coffers.!
Timo alifika alifika kwa plot haikua imefungwa main gate na akaingia nyumbani kitu saa nne.
Baba Timo:habari ya kushinda mwanangu?
Timo :poa mbuyu
Mama Timo :biashara vp?ali uliza proudly
Timo:karao wa kanjo mama
Wazazi waliangaliana,na Timo akawa angalia kimya chake kili sema yote,hawakutaka mengi juu haikua siku ya kwanza.
Mama Timo:mwanangu chakula hicho hapo,sisi twaingia kitandani
Baba Timo alimfuata wife.na wazazi wakingia nyuma ya curtain,palipo kua na kitanda.
Mama Timo:ukimaliza asha mosquito coil,na usisahau kuzima stima
Timo :sawa mama
Timo ali ji serve food ,na akashangaa bro yake alikua amekondoa macho haja lala
“Wewe Toni watoto wa rika yako wadooze”una wait nini?
“Umeniletea nini Timo?” Toni ali –ask na whisper
Mama Timo:Timo huja lala nikishuka utanijua,na wee Timo uamke mapema chukua pesa hapo chini ya radio,uende gikomba mapema ununue sanduku,tunaenda shule boarding kesho.
Timo alifinyia bro yake macho na kujifunika ,sara sista yake alikua next na yeye,na alikua slumberland aking’orota.baada ya nusu saa,Timo ali asha candle akazima stima,akazima radio,na kudooze.



Morning K-town ilikua radiant,clear sky na patches za clouds hapa na pale,watoi busy wakienda chuo ,mama mbogas wakirudi kutoka soko,raia ya industrial area,jeshi mathree taking over the street,pia wasee wa kurauka kwa vichinjio,Daggoreti.Njiru,Kiamaiko,na Burma pia wako busy na bike ama gari zao za color red na black,wote wako njiani yani wote wote wako kwa streets, Civil servants, Doctors, lawyers ,entrepreneurs, hawkers, street preachers, con artist, real artist wote wame-rise early in the name of national building,residents ama citizens wa k town ni hard working sana.
Timo alirauka ngware na kueleka kwa stage,soon matatu ilikuja
“Evereday day am hustling,This is Hepta entertainment….Dj mantrix on the mix .Plasma screen illi-annouce loud and clear.Air fresh ya perfume ili pata Timo ku-checki side alipata smile na alikua  mshe wa -power,
Timo: “sasa unaenda wapi ?asubuhi hii!
Msichana: “Nani amekuambia nataka kubonga na wewe?
Timo “Oohh pole!ali-apologise
“narudi kwetu na enda shule kesho ”alisema na kunyamaza
“umeitwa shule gani?Timo aliuliza
Alivunjia Timo kutoka kwa kiatu hadi kichwani alafu reluctantly ,
“unaitwa nani na unataka nini?
‘Timo” alisema
“mr Timo naitwa suzy na sitaki story mob,sawa?xaxa ni saa ngapi?ni mapema sana.
Timo ali –give up,na kuendelea kuangalia inje na soon,matatu ilipata huruma,air force,na ikafika eastleigh.
Matatu na magraffitti,majina kali kali ka,Field marshal Kimathi,street soldiers,rebel ,Harlem,mafia squand,black militias,street theatres,watu ka siafu waki –kriss cross street,mabuda na ma-kanzu,wamatha na bui bui,mashory na hipsters machali na hoods,ilikua ndio sight.scent kwa hewa ilikua tamu tamu ya biriani ,spices kutoka kila corners,clothing ,perfumes ,electronic shops zilikua dominant,sound kwa hewa ilikua horns za number tisa,na kutoka kwa loud speaker.za traders,just like k town  resident watu huku walikua hard working sana,but the same officio cartel activities zilikua dorminat hapa.un collected garbage all over even next to a military air base camp,roads zimejaa pot holes,
Jua ilikua pia ina take position kwa sky,ma-doves kibao zili-fly na ku-stand kwa wire ya stima,mat ilipita main road past Mater hospital,Eastleigh,every side ilikua na state of art shopping malls na pia ,kulikua na mosque biggie hiyo area.


Matatu ilipita California,na baadaye ikafika Gikomba Open air Market.As early as nine morning,kuna preacher ana preach aki move to and fro distance ya fifty metres,side zote ni highrise vendors,waki arrange merchedise wares zao,,
“Habari mathee”Timo alisalimiana
“Sema
“ nikuzie nini?
“Nitaka sanduku ya shule
Vendor: Karibu mwanangu unataka gani?
Anachecki checki na ku-point moja
Hii ni pesa ngapi?
Vendor: Mia nane baba
“Mimi nina mia sita”
Vendor: Ongeza mia baba
“Sina’
Vendor: Ulipewa ngapi na Baba
“Nilipewa mia sita na mama,tafadhali nuizie hivo sina haki sina”,
Vendor:Sawa baba leta,we we ni kijana wangu
Timothy Karanja alinunua box ya blue,na akaweza ku-save mia tatu,mamake alikua amempatia mia tisa,alirudi nyumbani na mamak akampeleka jenga hekima high school,huko aliendelea kusoma ,huku akipendwa na wanafunzi na waalimu,by the time afike form 4 alikua assistant school captain,na form four akiwa kaa skool captain aliongoza shule,kwa busara,na matokeo ya lipo tokea ya a mtihani wa Kenya certificate of secondary education(KCSE)
Mama yake alikua proud sana akiwambia wenzake ,mwanawe alikua kati ya wale wanafunzi wali perform poa nchini kote,na pia moja ya bank ilikua ready kungalamia masomo yake yote.

Baada ya miaka kadhaa
.
Sky  ilikua radiant,clear sky na patches za clouds hapa na pale,watoi busy  wakienda chuo ,mama mbogas  wakirudi kutoka soko,raia ya industrial area,jeshi   mathree taking over the street,pia wasee wa kurauka kwa vichinjio,Daggoreti.Njiru,Kiamaiko,na Burma pia wako budy na bike ama gari zao za color red na black,wote wako njiani yani wote wote  wako kwa streets, Civil servants, Doctors, lawyers ,entrepreneurs, hawkers, street preachers, con artist, real artist wote wame-rise early in the name of national building,residents ama citizens wa dee phase ni hard working sana.
.
Timo ali-take a glance over  shoulder.baadaye aka checki-watch na ku-realize ailikua amechelewa,ali-give up kum-chill,na aka- turn na kuanza ku-walk,kaa kwaida street ilikua na watu kibao kila mtu akiwa busy na kitega uchumi chake,ali-pass ma-shops ma-salons,ma butchery na of course bars.
alifika stage na kuchukua Matatu ya first ku-come,alli-take seat kwa window,alianza ku-checki  ma-potraits za mean looking faces za American celebs and Divas wamevaa sura ya kazi, kila side nikaa wana grudge,feeling ilikua nika uko club flashy neon lights of miscellaneous colors,soft velvet  seats

Song: Blak market  jua cali feat mejja.. wahuu nameless .Nu-linga nulinga ya elephant man ,Tanzania A li kiba  American Lil weezy,Rick ross
“Evereday day am hustling,This is Hepta entertainment….Dj mantrix on the mix .Plasma  screen illi-annouce loud and clear.Air fresh  ya perfume ilini-gonga ku-checki side nilipata bonge la smile na alikua wa-power
“sasa unaenda colle?Timo ali-ask
“Nani amekuambia na college?
“Oohh pole!ali -apologise
“Natafuta job”alisema na kunyamaza
“Naweza ona papers just in case”
Alivunjia Timo  kutoka kwa kiatu hadi kichwani alafu reluctantly akatoa brown envelope na kumipatia academic papers,Timo ali-shangaa na what he saw
Master of  business administration periyary university
Post graduate   accounting
Followed by other   list of other qualificatios
From primary school alikua student wa straight A’s
“sista hii university iko wapi?ali-ask
“Iko India,siku-manage kupata job huko juu sikua najua ku-speak ki-indree”ali  show Timo
“na una survive aje huku Nairobi?
“Mimi hutengeneza liquid soaps na kuuza kwa plots,hotels ,shules na sometimes hospitals..sista  ali- explain.
“okay nipee email yako just in case niskie mazuri”alimpatia hope
“sawa”ali whisper.
Kuchecki  ije  alikua ashapitishwa stage ,
Ali  move forward.
“wee shukisha,ali -command concodi ki-commander
“leta pesa kwanza,ulikua umelala!konkodi alizusha
“unajifanya migingo ung’ang’aniwe na nani:
:Ukichelewa  nunua yako tembea na Yesu kijana !
Timo ali tuliza na ku avoid ngori alikua ashazoea raia ya kuharibu siku
By this time Baba Timo alikua asha mwoa Waithera,na kuhama nyumbani,mama Timo alijikaza kisabuni na wanawe,na success yao yoyote ilikua sweet kwa soul yake.
Young man Timothy aliendelea kusaidia mamake Biashara na soon ikapanuka kwa muda mfupi sana,masomo pia alitia biidii katika chuo kikuu huku akijihusisha na biashara..alitembelea Benki Ya equity na kupata mkopo,na akkaweza kufungua nduka la kuuza nguo mpya katika street ya Kimathi mjini Nairobi..Hiyo ndiyo hadithi.ama kama hujani pata story ya before ya Mr Timo Karanja,mwana biashara mashuhuri,mwenye Timclads wear moi avenue,Tim electronics ltd, Timo Hardware ,na mumiliki wa Mother&Son boutique.
Bwana Timo alikua ame spend two hours akifanyisha watu interviews,aka shortlist wawili,Suzzy  Waruguru,na Jacob Mutua.Timo aliamua kuanza na Carol,alifungua makratasi yake,na kumkaribisha kwa offisi
Master of Business Administration Periyar University
Post graduate accounting
Followed by other a list of other qualificatios
From primary school alikua student wa straight A’s
“sista hii university iko wapi?Timothy ali ask
“Iko India,siku-manage kupata job huko juu sikua najua ku-speak ki-indree”carol replied
“na una survive aje huku Nairobi?Timo akauliza
Mimi hutengeneza liquid soaps na kuuza kwa plots,hotels ,shules na sometimes hospitals..sista ali- explain.
Thoughts za Timo zili flash back na aka kumbuka ali meet mrembo flani kwa matatu miaka tano iliisha –ma time ali kua ana hustle na ku hawk vitu .manze njo huyu ni Yule dame ali mshow anaitwa Suzzy!ali shikwa na mshangao kimoyo moyo-na huruma vile someone angechukua miaka tano bila works

“okay umenifurahisha sana kesho report kazini,but kabla Suzzy ya works to meet for coffee
“oooohhhhwwwiii Carol alijump “asante”ali whisper.Oh MyGod ni wewe Timo !huku aki tiririkwa na machozi.
Timo ali mu escort kwa mlango-na kuendelea na wengine.siku iliyo fuata Timo alirauka ngware kama kawa akiwa amechangamka sana.

 ‘ukikataa utaniumiza kukupenda sitaweza”
Unanielewa mbona unachelewa mbona”
Niambie nije nije sasa hivi”
Song ya mbongo flava ilikua inachuna kutoka kwa streo speakers mdogo mdogo,place yenyewe ilikua imetulia sana,murmurs na whisper ndio ilikua code za conversation,café dela crème ilikua joint new Moi Avenue ,perfect haven ya raia ya middle class,haikua na swagg mob ka the rest za uptown,wasee hapa walikua less complex and real.
Timo hakua ameachwa nyuma ,na hio ndio place wali-have first date ,na ilim-take mbaya,within mwezi moja alikua ashaanua Suzzy,na kupiga rubber stamp.
Ali inua mkono na kuitisha expresso double,ya pilli,alikua asha kaa one hour waiting in vain,Suzzy alikua anakaa time keeper mbaya,Timo alishangaa.alijipa shughuli na kuanza kuangalia abstract picture kali zilikua kwa wall,halafu aka-decide ku-log kwa facebook,alichomoa Tablet phone,aka –login kwa facebbook,
Timo na Ngori Za Mtaa- SHENGseries imechorwa na Mwas Mahugu
To be continued.

No comments:

Post a Comment